Posts

Je, ni sahihi kusali sala kwa kurudia rudia mfano Novena?

Ndiyo, Hii ni kwa sababu sala nyingi za kurudia ni za Ahadi na zinasaliwa ili kutimiza ahadi ile. Mfano Novena husaliwa kwa siku 7 au 9 kwa nia ya kupata kile kilichoahidiwa au kinachodhamiriwa. Mungu alishawahi kuwaagiza Waisraeli wafanye Ibada maalumu kwa kurudiarudia mfano wakati walipoangusha kuta za Yeriko walifanya Ibada maalumu kwa siku 7 (Saba). "Waisraeli walipopita waliagizwa na Mungu kuzunguka Mji wa Yeriko 2Kisha BWANA akamwambia Yoshua,“Tazama, nimeitia Yeriko mikononi mwako, pamoja na mfalme wake na watu wake wa vita. 3Zunguka mji mara moja pamoja na watu wako wote wa vita. Fanya hivi kwa siku sita. 4Uwe na makuhani saba wakibeba mabaragumu ya pembe za kondoo waume mbele ya sanduku. Siku ya saba, mzunguke mji mara saba, nao makuhani wakipiga baragumu hizo. 5Utakaposikia makuhani wamepaliza sauti kubwa ya baragumu, watu wote wapige kelele kwa sauti kuu, kisha ukuta wa mji utaanguka na watu watakwea, kila mtu aingie ndani moja kwa moja kutokea pale alipo.’...

Biblia ni nini? Asili, Historia, waandishi na mipaka yake

  Biblia ni nini? Asili, Historia, waandishi na mipaka yake asili   biblia   kanisa   katoliki   madhehebu   mapokeo   mitume roho_mtakatifu   visakramenti   watakatifu Biblia ni mkusanyiko wa vitabu mbalimbali vinavyohusu kazi ya Mungu ya kuwakomboa mwanadamu Je, Biblia ilipatikanaje? Nini chanzo na asili ya Biblia. Biblia iliundwa kwa kukusanya vitabu vya dini vya wakristo hapo awali na kuunda kitabu kimoja. Kwa maana hii ni kwamba Biblia ni vitabu teule vya dini na hivyo vipo vitabu vingine vya dini ambavyo havikuwekwa Kwenye Biblia. Kwa hiyo basi Wakristo wa kwanza walichagua vitabu kadhaa na kuviweka pamoja na kisha kuvita Biblia. Biblia ni mkusanyiko wa vitabu muhimu tuu vya dini mpaka kufikia Enzi za Mitume. Je, Biblia ndicho kitabu pekee cha neno la Mungu? Hapana, Biblia sio kitabu pekee cha neno la Mungu isipokua Biblia ni kitabu kilichoidhinishwa rasmi kutumika Kama kitabu kikuu cha Wakristo. Hii ni kwa sababu Biblia imeundwa ...

KWA NINI UKAKATA TAMAA?

Kwa nini tunakata tamaa? Katika maisha kila mmoja anakuwa na malengo fulani, na kama wakristo wote tunalo lengo moja la kuufukia ufalme wa Mungu. Katika safari hii wapo tulioanza nao ila kwa sababu kadha wa kadha wamerudi nyuma na wapo wanakaribia kurudi nyuma. Kitendo cha kuona hamna njia tena wala uwezekano wa kufanikisha jambo fulani twaweza kukiita kama  kitendo cha kukata tamaa. Hali ya kutokutaka kuendelea wala kujaribu tena kufanya jambo hilo, kujihukumu nafsi yako  na kutaka hata kutokukumbuka tena jambo hilo, kukosa kiu ya kujaribu tena. Huko ni kukata tamaa. Kuachana na elimu pia kuna yale malengo ya kimaisha mfano miito ya kimaisha na ila ya kanisa. Wapo waliofika ngazi fulani katika ndoto zao wakakata tamaa, wengine walifika hatua karibu na mafanikio kabisa mfano mwaka wa kichungaji n.k, ila kwa sababu kadha wa kadh wamerudi nyuma. Kwanini watu wanakata tamaa? 1.Kutokuwa na mipango ya kimaisha au kitu unachotaka kufanya. Ni jambo la kawaida sana kwa watu wengi ...

MAZISHI MV NYERERE

Image
Shughuli ya Mazishi ya wapendwa wetu walioiaga dunia sept 20 ndio ipo katika taratibu ya kuhifadhiwa. Viongozi mbalimbali wa serikali, wananchi, na Viongozi wa dini na vyombo vya dola wanahudhuria shughuli hii.

MASOMO YA MISA, SEPTEMBA 23, 2018 DOMINIKA YA 25 YA MWAKA B

Image
MASOMO YA MISA, SEPTEMBA 23, 2018 DOMINIKA YA 25 YA MWAKA B INJILI Mk. 9:30-37 "Wakatoka huko, wakapita katikati ya Galilaya; naye hakutaka mtu kujua. Kwa sababu alikuwa akiwafundisha wanafunzi wake, akawaambia, Mwana wa Adamu yuaenda kutiwa katika mikono ya watu, nao watamwua; hata akiisha kuuawa, baada ya siku tatu atafufuka. Lakini hawakulifahamu neno lile, wakaogopa kumwuliza. Wakafika Kapernaumu; hata alipokuwamo nyumbani, akawauliza, Mlishindania nini njiani? Wakanyamaza; kwa maana njia walikuwa wakibishana wao kwa wao, ni nani aliye mkubwa. Akaketi chini, akawaita wale Thenashara akawaambia, Mtu atakaye kuwa wa kwanza atakuwa wa mwisho kuliko wote, na mtumishi wa wote. Akatwaa kitoto, akamweka katikati yao, akamkumbatia, akawaambia, Mtu akimpokea mtoto mmoja wa namna hii kwa jina langu, anipokea mimi, na mtu akinipokea mimi, humpokea, si mimi, bali yeye aliyenituma." Tafakari fupi! " atakaye kuwa wa kwanza atakuwa wa mwisho kuliko wote na m...

HISTORIA YA HAYATI BABA WA TAIFA MWL. JULIUS NYERERE

Image
(Hayati Mwl. Julius K. Nyerere) Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa raisi wa kwanza wa Tanzania, alizaliwa Butiama mkoani Mara mnamo tarehe 13 April 1922 na alifariki dunia 14 Oktoba 1999. Alikuwa mojawapo kati watoto 26 wa Nyerere Burito, chifu wa kabila la Wazanaki. Alipokuwa mtoto Nyerere alichunga mifugo ya babake; katika umri wa miaka 12 aliingia shule akitembea kilomita 30 hadi Musoma. Baada ya kumaliza shule ya msingi aliendelea kusom a shule ya wamisionari Wakatoliki huko Tabora. Katika umri wa miaka 20 alibatizwa akawa mkristo Mkatoliki hadi mwisho wa maisha yake. (Mama Maria Nyerere, mke wa Hayati baba wa Taifa) Mapadre wakaona akili yake wakamsaidia kusoma ualimu huko Makerere, Kampala, Uganda kuanzia 1943 - 1945. Makerere akaanzisha tawi la Umoja wa wanafunzi Watanganyika pia amejihusisha na tawi la Tanganyika African Association (TAA). Baada ya kumaliza masomo ya ualimu alirudi Tabora akifundisha shule ya St.Mary´s. Mwaka 1949 alipata skolashipu ya kwenda kusoma ...