MASOMO YA MISA, SEPTEMBA 23, 2018 DOMINIKA YA 25 YA MWAKA B

MASOMO YA MISA, SEPTEMBA 23, 2018
DOMINIKA YA 25 YA MWAKA B

INJILI
Mk. 9:30-37

"Wakatoka huko, wakapita katikati ya Galilaya; naye hakutaka mtu kujua. Kwa sababu alikuwa akiwafundisha wanafunzi wake, akawaambia, Mwana wa Adamu yuaenda kutiwa katika mikono ya watu, nao watamwua; hata akiisha kuuawa, baada ya siku tatu atafufuka. Lakini hawakulifahamu neno lile, wakaogopa kumwuliza.
Wakafika Kapernaumu; hata alipokuwamo nyumbani, akawauliza, Mlishindania nini njiani? Wakanyamaza; kwa maana njia walikuwa wakibishana wao kwa wao, ni nani aliye mkubwa. Akaketi chini, akawaita wale Thenashara akawaambia, Mtu atakaye kuwa wa kwanza atakuwa wa mwisho kuliko wote, na mtumishi wa wote. Akatwaa kitoto, akamweka katikati yao, akamkumbatia, akawaambia, Mtu akimpokea mtoto mmoja wa namna hii kwa jina langu, anipokea mimi, na mtu akinipokea mimi, humpokea, si mimi, bali yeye aliyenituma."

Tafakari fupi!
" atakaye kuwa wa kwanza atakuwa wa mwisho kuliko wote na mtumishi wa wote"
Yesu anawaonya Thenashara wake juu ya ukuu na nani apaswa kuwa mkubwa na kwa mastahili yapi. Anamtaja wa mwisho na mtumishi wa wote ndiyo mkubwa. INJILI ya Leo yatugusa sana upande wa utawala na uongozi. Pasipo kuwa mtumwa wa wengine hakuna upendo. Msingi wa Yesu kumtaja aliye mkubwa kuwa ndiye mdogo unajikita katika upendo na upendo ni maana yake kwa ajili ya wengine na si binafsi. Mitume waliwaza nani atakuwa mkubwa na kukaa wapi hawakuwaza nani atahubiri na kwatumikia maskini wapi. 

Hakika kanisa linapaswa kuwa la chini kabisa yaani nyumba ya maskini na mjane na yatima, kupitia kwako mkristu lazima tujishushe kama kanisa kwa ajili ya dunia yenye mahitaji kadha wa kadha, tujishushe sana kwatumikia wengine na Mungu atatuinua siku ya mwisho. Anayempokea maskini amempokea Yesu na Mungu mwenyewe kwani Maskini tupo nao siku zote ila Yesu ni kwa muda tu.

Mtoto mdogo siku zote hukimbilia msamaha akikosea, hachukii watu kwa muda mrefu, hahesabu uadui, hahesabu hadhi yake bali hucheza na kukaa na mtoto yoyote ajaye kwake. Nasi tukiwa kama watoto ufalme ni wetu. 

Sifa nguvu na utukufu vi nawewe Mungu wetu milele yote. Amia

Kwa jina la Baba, na La Mwana na La Roho Mtakatifu. Amina. 

@katolikiTanzania

Comments

Popular posts from this blog

Biblia ni nini? Asili, Historia, waandishi na mipaka yake

HISTORIA YA HAYATI BABA WA TAIFA MWL. JULIUS NYERERE