KWA NINI UKAKATA TAMAA?
Kwa nini tunakata tamaa?
Katika maisha kila mmoja anakuwa na malengo fulani, na kama wakristo wote tunalo lengo moja la kuufukia ufalme wa Mungu. Katika safari hii wapo tulioanza nao ila kwa sababu kadha wa kadha wamerudi nyuma na wapo wanakaribia kurudi nyuma. Kitendo cha kuona hamna njia tena wala uwezekano wa kufanikisha jambo fulani twaweza kukiita kama kitendo cha kukata tamaa. Hali ya kutokutaka kuendelea wala kujaribu tena kufanya jambo hilo, kujihukumu nafsi yako na kutaka hata kutokukumbuka tena jambo hilo, kukosa kiu ya kujaribu tena. Huko ni kukata tamaa.
Kuachana na elimu pia kuna yale malengo ya kimaisha mfano miito ya kimaisha na ila ya kanisa. Wapo waliofika ngazi fulani katika ndoto zao wakakata tamaa, wengine walifika hatua karibu na mafanikio kabisa mfano mwaka wa kichungaji n.k, ila kwa sababu kadha wa kadh wamerudi nyuma.
Kwanini watu wanakata tamaa?
1.Kutokuwa na mipango ya kimaisha au kitu unachotaka kufanya. Ni jambo la kawaida sana kwa watu wengi kutokuwa na mipango ya kimaandishi au rasmi kwa ajili ya vitu fulani katika maisha yao. Wengi hujikuta wanakosa mwelekeo hasa kwenye magumu na kushindwa kujua wapi na lini walitakiwa wafanye nini, mwishowe hushindwa kabisa la kufanya na kuamua kukata tamaa kwani hawalewi kipi kilifanyikaje na wapi palikosewa na lini kilifanyika..1 Wakorintho 14 [40]Lakini mambo yote na yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu.
2.Kuiga maisha au njia za kukufanya ufanikiwe. Kila mtu ana mpango binafsi wa majsha alikwisha kuandikiwa na Mungu hivyo kuiga mipango ya wengine ni kujipotezea muda. Huwezi ukauiga mpango wa maisha wa mtu aliyezaliwa na kuishi maisha ya tofauti na wewe. Utakuja kuona baadhi ya vitu alivyopitia yeye vinakosekana katika maisha yako na hivyo njia yake sio sawa tena na ya kwako, unaona ugumu na vitu haviendi tena unakata tamaa ya kuendelea mbele.
3.Kuwasikiliza walioshindwa au kukata tamaa. Maneno ya waliokata tamaa hujaa mbinu za kushindwa na ubatili mtupu. Wao hukunbuka kushindwa kwao na kuona unafuu wakukata tamaa kuliko kuendelea. Wachache sana watakao kupa moyo ila wengi watapenda ushindwe kama wao. “hutoboi” “labda sio hapa duniani” “wameshindwa wengine we utaweza” Maneno yao hukatisha tanaa mara dufu, tafuta waliofanikiwa
4.Kukosa wafariji au watu wa kukutia moyo. Tunapopitia matatizo makubwa hua tunahitaji watu wa kutufariki na kututia moyo, watu wa kuendelea kutuambia tunaweza tuendelee hata pasipo kukusaidia kwa mali ila kwa hali tu. Watu wa kutusaidia hata kufanya vutu fulani fulani, pale tunapokosa tunajihukumu kama wakosaji na wasio faa mbele ya jamii na kuamua kukata tamaa. Yohana 5 [7]Yule mgonjwa akamjibu, Bwana, mimi sina mtu wa kunitia birikani, maji yanapotibuliwa; ila wakati ninapokuja mimi, mtu mwingine hushuka mbele yangu.
5.Kuishi na watu wasiojua thamani yako na unachofanya. pale unapokaa na watu wasio thamini unachofanya na kukuchukulia mjinga hua ni kikwazo kikubwa. Wengine wanakucheka kwa unachofanya na kukuita majina ya kukughadhabisha na kutaka kukutoa katika njia uliyopo. Wakati mwingine tunatengwa kabisa na watu fulani kwa kuona hiki tunachofanya si cha thamani. Mwishowe tunaona tofauti yetu na jamii tunaona suluhu ni kukata tamaa.
6.Kuyumba kiimani na kushindwa kumwamini Mungu wa kweli. Pindi tunapoomba tunategemea mara zote tupate toka kwa Mungu. Tunapoona kama maombi hayajibiwi au kuhisi kama Mungu hayupo tunayumba kiimani na kushindwa kuamini tena katila msaada wa Mungu na kuajaribu kwenda peke yetu. Pale imani inapoyumba nasi pia tunayumba na mambo yetu yanayumba mwishowe tunaona hakuna namna ila kukata tamaa na tunachokifanya. Matendo ya Mitume 27: [20]Jua wala nyota hazikuonekana kwa muda wa siku nyingi, na tufani kuu ikatushika, basi tukakata tamaa ya kuokoka.
7.Kuisikiliza nguvu na sauti ya shetani. Siku zote unapoanza safari kuelekea mafanikil mema kuna sauti kubwa itakwambia huewezi aidha toka ndani au nje (kwa wandamu) itakwambia hamna wepesi katika hili. Hii ni sauti ya shetani mwovu. Sauti yake huchosha masikio ya nafsi kwani kila unapotaka kujaribu yenyewe hukujia na kukuvunja moyo na usithubutu kujaribu. Wapo wanaoisikiliza hii na kuipuuza ile ya ukweli inayofariji kwa upole sana ikikupa moyo zaidi. Mfano shetani anamjaribu Yesu kabla ya kuanza kazi ya ukombozi.
8.Kutumia njia za mkato. Njia za mkato zina mwisho wake kwani sio za halali, huwa na changamoto zake nyingi japo huonesha mafanikio yapo karibu sana. Hapa utakutana na magumu makubwa kama mikono na hukumu za sheria, mara nyingi hua ni njia za kuiga hivyo huhitaji ujuzi mwingi sana kiakili, hivyo unapoona mambo hayaendi kulinganisha na tamaa yako ya kufanikiwa unajikuta unakosa Jinsi zaidi unakata tamaa.
9.Kujihisi ni wa hali ya chini kimaisha. Hali mbaya za kiuchumi hupelekea watu kushindwa hata kujaribu kufanya lolote kwa kuhisi hali zao zitawalwamisha baadae katika safari zao za kimaisha.
10.Kukumbuka yaliyopita na kuhukumu kesho kupitia jana yako. Watu wengi hukumbuka jana ilivyokuwa na Kukumbuka walioshindwa na kuabika, kuhisi mambo ya kesho yatakuwa vivo hivyo. Huenda ikawa ni kwa kumtizama ndugu au rafiki yako alivyopitia magumu, au ulivyowahi kupitia ugumu katika maisha yako. Kumbukumbu za magumu ya jana husononesha nafsi na kuhukumu kila unaloamua katika njia zenye ukali ndani yake. Kumbukumbu za yaliyopita hufanya wengi kutojaribu tena na kukata tamaa.
11.Vipingamizi toka kwa wakubwa wako. Watu unaowategemea hasa wanafamilia (wazazi na ndugu wa karibu) wanapokwambia hili haliwezekani, Maneno yao hua yana nguvu sana kutuhamisha kwenye lengo letu. Familia ndio nguzo ya kwanza ya kukuelekeza na kukupa moyo katika maamuzi yako unayochukua. Pale wanapokuwa wakwanza kukuvunja moyo basi utaghalifika mapema sana. Wapo wengi sana walioshindwa kuendelea na mipango yao ya kimaisha na kutata tamaa kabisa. Wakolosai 3:[21]Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa.
12.Kutazama na kuamini magumu zaidi kuliko wepesi. Watu wengi huona magumu yaliyoko mbele yao na kusahau mbele zaidi kuna nini, hutizama magumu na kuamua kuwa hatutopita salama, tunaona magumu hatuoni njia, tunaona heri shari kuliko nusu shari, tunakata tamaa. Pengine kuna mambo makubwa tunayohisi yatazidi uwezo wetu na njia zetu zote au au kisikia tu magumu toka kwa watu wengine, tunayumbishwa katika msimqmo. Na tunakata tamaa ya kuendelea tena. una2 Wakorintho 1:[8]Maana ndugu, hatupendi, msijue habari ya dhiki ile iliyotupata katika Asia, ya kwamba tulilemewa mno kuliko nguvu zetu, hata tukakata tamaa ya kuishi.
13.Kukosa uvumilivu na kusahau raha ya mafaniko. Wengi wengine hushindwa kuvumilia magumu ya maisha, hasara za magumu hayo na kuona mambo yote ni maumivu na hasara tupu, hamna haja kuendelea tena kwani ni dhahiri kuwa mambo hayo huumiza sana na kuvunja moyo.
14.Kutegemea watu wengine au vitu fulani. Pindi tunapotegemea watu wengine katika kutimiza mambo yetu inapotokea watu hao wanatuonyesha ushirikiano mdogoa au kukumbana na vikwazo kutusaidia, tunajikuta tupo peke yetu na tumepungukiwa nguvu muhimu sana pembeni yetu. Tunajikuta hatuwezi kuendelea tena tunakata tamaa kwani msaada wetu haupo tena nasi.
Ushauri wangu kwako!
Bado safari ni ndefu kuufikia uzima wa milele, Damu Ya Kristo ilimwagika kukamilisha ushindi huu. Jisafishe kwa damu hiii utapita magumu yote na kufurahia ushindi.
Tatizo sio Mungu wala watu wengine wala shetani, tatizo ni wewe mwenyewe, anza upya w. Usiogope maneno wala vitisho vya hao waliwahi kushindwa, mguekie Mungu jikabidhi wewe na mipango yako naye ataibariki. Usihukumu nafsi yako unapodondoka, tazama kisiki kilichokudondosha kiondoe, chunga ukikutana na kama hicho usijikwae tena. “quit when you are done not when you are tired” sahau kuhusu jana yako kwani haina cha kufanya kwa ajili ya kesho yako, lakink unaweza kufanya kitu sasa kwa ajili ya kesho. Stop the series of hurting memories, start new ones and plan to archive something great to celebrate for it tomorrow. Stop re-reading the last chapter to read the next one of your life. Forget all what happened in the past, do something for tomorrow. Yote tunayofanya lazima tumtangulize kwanza Mungu kwani yeye atakuwa mfariji wetu na atatutia nguvu hata mwisho wa ushindi. Fanya maamuzi sahihi, muite na Roho. Mtakatifu, Sali kabla ya kuanza na hata wakati wa kutimiza lengo. I pray that you will never give up, remember this voice “U CAN”. Isikilize sauti ya Mungu inayokuita na kukutia nguvu achana na yote msikilize yeye. Mwisho wa yote utukufu sifa na ukuu ubaki kwa Mungu Mwana, Mungu roho mtakatifu, na enzi ni yake Mungu Baba. Amina.
MWISHO
“NEVER GIVE UP, U CAN DO IT”
Comments
Post a Comment