Posts

Showing posts with the label semina

Mambo yanayoweza kusababisha sala au maombi yako yasijibiwe

Image
Mara nyingi tumekua tukiomba lakini hatupati, sababu zinaweza zikawa hizi ; 1. Mawazo na matarajio yetu Mara nyingi tunajifunga kwenye maombi yetu pale tunapoomba na kisha kuanza kuwaza "hivi Mungu atanipa kikubwa au kidogo au atanisaidia sana au kidogo" Au tunaomba halafu tunakua na matarajio tofauti na kile tunachoomba. Aidha tunatarajia kupata kidogo au kikubwa. Hali hii ni sawa na kumuwekea Mungu kizuizi kwenye maombi yako. Yaani kumuongoza Mungu afanye kwa kiasi kile unachofikiri. 2. Kulenga kutizamwa na watu. Hii ni kuomba kwa majivuno yaani kuomba ili ukishapata watu waone kuwa umepata. Jambo hili linamchukiza Mungu ndio maana unapoomba kupewa kitu au kusaidiwa kitu Mungu hafanyi /hakupi. Na Mara nyingine hata vile ulivyonavyo unanyan'ganywa kwa kuwa hauombi kwa utukufu wa Mungu bali kwa utukufu wako. Hali hii ni sawa na kumuwekea Mungu ukuta kwenye maisha yako. Namna njema ya kuomba ni hii 1. Kutokuomba mambo makuu sana ambayo huna haja nayo na hayana ma...

KWA NINI UKAKATA TAMAA?

Kwa nini tunakata tamaa? Katika maisha kila mmoja anakuwa na malengo fulani, na kama wakristo wote tunalo lengo moja la kuufukia ufalme wa Mungu. Katika safari hii wapo tulioanza nao ila kwa sababu kadha wa kadha wamerudi nyuma na wapo wanakaribia kurudi nyuma. Kitendo cha kuona hamna njia tena wala uwezekano wa kufanikisha jambo fulani twaweza kukiita kama  kitendo cha kukata tamaa. Hali ya kutokutaka kuendelea wala kujaribu tena kufanya jambo hilo, kujihukumu nafsi yako  na kutaka hata kutokukumbuka tena jambo hilo, kukosa kiu ya kujaribu tena. Huko ni kukata tamaa. Kuachana na elimu pia kuna yale malengo ya kimaisha mfano miito ya kimaisha na ila ya kanisa. Wapo waliofika ngazi fulani katika ndoto zao wakakata tamaa, wengine walifika hatua karibu na mafanikio kabisa mfano mwaka wa kichungaji n.k, ila kwa sababu kadha wa kadh wamerudi nyuma. Kwanini watu wanakata tamaa? 1.Kutokuwa na mipango ya kimaisha au kitu unachotaka kufanya. Ni jambo la kawaida sana kwa watu wengi ...