Mambo yanayoweza kusababisha sala au maombi yako yasijibiwe
Mara nyingi tumekua tukiomba lakini hatupati, sababu zinaweza zikawa hizi ;
1. Mawazo na matarajio yetu
Mara nyingi tunajifunga kwenye maombi yetu pale tunapoomba na kisha kuanza kuwaza "hivi Mungu atanipa kikubwa au kidogo au atanisaidia sana au kidogo" Au tunaomba halafu tunakua na matarajio tofauti na kile tunachoomba. Aidha tunatarajia kupata kidogo au kikubwa.
Hali hii ni sawa na kumuwekea Mungu kizuizi kwenye maombi yako. Yaani kumuongoza Mungu afanye kwa kiasi kile unachofikiri.
2. Kulenga kutizamwa na watu.
Hii ni kuomba kwa majivuno yaani kuomba ili ukishapata watu waone kuwa umepata.
Jambo hili linamchukiza Mungu ndio maana unapoomba kupewa kitu au kusaidiwa kitu Mungu hafanyi /hakupi. Na Mara nyingine hata vile ulivyonavyo unanyan'ganywa kwa kuwa hauombi kwa utukufu wa Mungu bali kwa utukufu wako.
Hali hii ni sawa na kumuwekea Mungu ukuta kwenye maisha yako.
Namna njema ya kuomba ni hii
1. Kutokuomba mambo makuu sana ambayo huna haja nayo na hayana maana katika maisha yako.
2. Kutokuomba mambo madogo kwa mawazo labda nikiomba makubwa Mungu hataweza
3. Kutokuomba kwa ajili ya kutaka kuonekana na watu.
Tumsifu Yesu Kristo. Usisahau kushare ujumbe huu mzuri na wapendwa wako.
Comments
Post a Comment