Posts

trending

FAHAMU HUDUMA YA UTOAJI MAPEPO (EXCORCISM) KATIKA KANISA KATOLIKI. N a Wileha rd Maro Niliye mdogo kuliko wote. Lipo swali au shutuma juu ya kanisa katoliki kuwa “wakatoliki hawatoi mapepo kama alivyofanya Yesu” basi leo tuichambue huduma hii katika kanisa katoliki. Kwanza ni wazi kuwa kanisa katoliki linatoa huduma hii kwa waamini wanaothibitika kushikiliwa na nguvu za kishetani (demonic possession) kwa kuondoa nguvu hizo kwa jina la Yesu. Katekisimu ya Kanisa Katoliki namba 1673 inaeleza kuwa kupunga pepo kunaelekezwa katika kumfukuza shetani au ukombozi dhidi ya kupagawa na pepo na kupitia kwa mamlaka ya kiroho ambayo Kristo amelikabidhi Kanisa. Mara nyingi huduma hii haifanyiki kwa uwazi au mbele ya kusanyiko kama ilivyo kwa baadhi ya madhehebu ya kipentekoste na kiprotestanti hivo kufanya ionekane kama huwa haifanyiki lakini ni kweli kuwa huduma hii inafanyika ndani ya kanisa katoliki. 1.       Kupunga pepo kulianza lini? Visa vya kupunga...

Mambo yanayoweza kusababisha sala au maombi yako yasijibiwe

Image
Mara nyingi tumekua tukiomba lakini hatupati, sababu zinaweza zikawa hizi ; 1. Mawazo na matarajio yetu Mara nyingi tunajifunga kwenye maombi yetu pale tunapoomba na kisha kuanza kuwaza "hivi Mungu atanipa kikubwa au kidogo au atanisaidia sana au kidogo" Au tunaomba halafu tunakua na matarajio tofauti na kile tunachoomba. Aidha tunatarajia kupata kidogo au kikubwa. Hali hii ni sawa na kumuwekea Mungu kizuizi kwenye maombi yako. Yaani kumuongoza Mungu afanye kwa kiasi kile unachofikiri. 2. Kulenga kutizamwa na watu. Hii ni kuomba kwa majivuno yaani kuomba ili ukishapata watu waone kuwa umepata. Jambo hili linamchukiza Mungu ndio maana unapoomba kupewa kitu au kusaidiwa kitu Mungu hafanyi /hakupi. Na Mara nyingine hata vile ulivyonavyo unanyan'ganywa kwa kuwa hauombi kwa utukufu wa Mungu bali kwa utukufu wako. Hali hii ni sawa na kumuwekea Mungu ukuta kwenye maisha yako. Namna njema ya kuomba ni hii 1. Kutokuomba mambo makuu sana ambayo huna haja nayo na hayana ma...
Image
Sala kwa Mkatoliki ni nini hasa? Tunaposema sala tunamaanisha nini  Sala ni kuongea na Mungu. Sala kwa Mkatoliki inajumuisha maombi, tafakari, ibada, taamuli, shukrani na sifa. Maana ya sala kwa Mkristo Mkatoliki sio kuomba tuu kama wanavyotafsiri watu wasio wakatoliki. Wengi wa wasio Wakatoliki wanaposema Sala wanamaanisha Maombi. Kwa hiyo kwa Mkatoliki, Sala ni zaidi ya Maombi. Ndiyo maana kwa mkatoliki kuna sala za namna mbalimbali kama vile za Tafakari, za Maombi za Sifa na za kushukuru. Mfano sala ya Atukuzwe Baba sio maombi bali ni sala ya kumtukuza Mungu kwa maana hiyo sio Maombi, ndiyo maana husaliwa baada ya sala au matukio fulani kama ishara ya kumtukuza Mungu na kutambua ukuu wa Mungu Yesu alifundisha tusali vipi? Kisha Yesu akawapa wanafunzi Wake mfano ili kuwaonyesha kuwa yawapasa kuomba pasipo kukata tamaa. 2Akawaambia, “Katika mji mmoja alikuwapo hakimu ambaye hakumwogopa Mungu wala kumjali mtu. 3Katika mji huo alikuwako mjane mmoja ambaye alikuwa ak...