Posts

Showing posts from March, 2020
FAHAMU HUDUMA YA UTOAJI MAPEPO (EXCORCISM) KATIKA KANISA KATOLIKI. N a Wileha rd Maro Niliye mdogo kuliko wote. Lipo swali au shutuma juu ya kanisa katoliki kuwa “wakatoliki hawatoi mapepo kama alivyofanya Yesu” basi leo tuichambue huduma hii katika kanisa katoliki. Kwanza ni wazi kuwa kanisa katoliki linatoa huduma hii kwa waamini wanaothibitika kushikiliwa na nguvu za kishetani (demonic possession) kwa kuondoa nguvu hizo kwa jina la Yesu. Katekisimu ya Kanisa Katoliki namba 1673 inaeleza kuwa kupunga pepo kunaelekezwa katika kumfukuza shetani au ukombozi dhidi ya kupagawa na pepo na kupitia kwa mamlaka ya kiroho ambayo Kristo amelikabidhi Kanisa. Mara nyingi huduma hii haifanyiki kwa uwazi au mbele ya kusanyiko kama ilivyo kwa baadhi ya madhehebu ya kipentekoste na kiprotestanti hivo kufanya ionekane kama huwa haifanyiki lakini ni kweli kuwa huduma hii inafanyika ndani ya kanisa katoliki. 1.       Kupunga pepo kulianza lini? Visa vya kupunga...