Posts

Showing posts from July, 2017

HISTORIA YA HAYATI BABA WA TAIFA MWL. JULIUS NYERERE

Image
(Hayati Mwl. Julius K. Nyerere) Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa raisi wa kwanza wa Tanzania, alizaliwa Butiama mkoani Mara mnamo tarehe 13 April 1922 na alifariki dunia 14 Oktoba 1999. Alikuwa mojawapo kati watoto 26 wa Nyerere Burito, chifu wa kabila la Wazanaki. Alipokuwa mtoto Nyerere alichunga mifugo ya babake; katika umri wa miaka 12 aliingia shule akitembea kilomita 30 hadi Musoma. Baada ya kumaliza shule ya msingi aliendelea kusom a shule ya wamisionari Wakatoliki huko Tabora. Katika umri wa miaka 20 alibatizwa akawa mkristo Mkatoliki hadi mwisho wa maisha yake. (Mama Maria Nyerere, mke wa Hayati baba wa Taifa) Mapadre wakaona akili yake wakamsaidia kusoma ualimu huko Makerere, Kampala, Uganda kuanzia 1943 - 1945. Makerere akaanzisha tawi la Umoja wa wanafunzi Watanganyika pia amejihusisha na tawi la Tanganyika African Association (TAA). Baada ya kumaliza masomo ya ualimu alirudi Tabora akifundisha shule ya St.Mary´s. Mwaka 1949 alipata skolashipu ya kwenda kusoma ...